Kenya na Lesotho zimejitolea kuimarisha ushirikiano wao katika kilimo ili kuongeza usalama wa chakula na uvumbuzi. Azimio hilo lilifikiwa wakati wa mazungumzo kati ya Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe na mwenzake kutoka Lesotho Selibe Mochoboroane. Viongozi hao wawili walijadili kuimarisha ushirikiano katika mifumo ya mbegu, kilimo cha bustani, maendeleo ya mifugo, kilimo kinachozingatia mabadiliko ya hali ya hewa, utafiti na uvumbuzi, kwa kuzingatia kuharakisha mabadiliko endelevu ya kilimo na kuboresha usalama wa chakula na lishe katika nchi zote mbili.