Kenya itawakaribisha zaidi ya wajumbe elfu 10 kutoka nchi 40 katika Maonyesho ya 16 ya Usafiri ya Magical Kenya, yaliyopangwa kufanyika Oktoba 6–8, mwaka huu, katika Bustani ya Uhuru jijini Nairobi. Hafla hiyo itawashirikisha zaidi ya waonyeshaji 400 na zaidi ya wanunuzi 250 wa kimataifa waliothibitishwa. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Nchini, June Chepkemei, alisema maonyesho hayo yanaangazia utayari wa Kenya kuendesha ukuaji wa utalii barani Afrika kupitia data, teknolojia na ushirikiano wa kimkakati wa kibiashara.

JUNE CHEPKEMEI - RELIANT