Bunge limehimizwa kuharakisha kupitisha Muswada wa Marekebisho wa Udhibiti wa Tumbaku ili kushughulikia bidhaa mpya za tumbaku, ikiwa ni pamoja na shisha. Mwenyekiti wa Muungano wa kuthibiti Tumbaku Joel Gitali anasema marekebisho hayo sasa ni ya dharura zaidi baada ya mahakama kutangaza marufuku ya shisha kuwa kinyume cha sheria, akiihimiza Wizara ya Afya kutegemea maamuzi yake kwa uungwaji mkono wa kisheria na sio umaarufu wa umma.
JOEL GITALI - LAW