Wazazi na wanafunzi walioathiriwa na kashfa ya elimu ya Finland ya Sh bilioni 1 walifanya maandamano mjini Eldoret jana, wakitaka kurejeshewa pesa zao. Waandamanaji hao walivamia makao makuu ya Kaunti ya Uasin Gishu wakitaka kukutana na Gavana Jonathan Bii kuhusu kashfa hiyo. Wazazi na wanafunzi hao walikuwa wamebeba mabango yakidai uongozi wa kaunti hiyo kuhakikisha wanarejeshewa pesa zao.