Tume ya kuajiri walimu TSC imefungua maombi ya nafasi elfu 20 za walimu katika Shule za Junior School katika kampeni mpya ya kuajiri inayolenga kusaidia utekelezaji wa Elimu ya CBE. Tume hiyo ilisema nafasi hizo zinapatikana kwa wagombea waliohitimu na maombi yatakubaliwa mtandaoni kuanzia Jumanne, Agosti tarehe 18, hadi Jumatatu, Agosti tarehe 31. Maombi ya kuwasilisha kwa mikono hayatakubaliwa.