Kocha mkuu wa Harambee Starlets, Beldine Odemba, anasema walizidiwa na Morocco katika mechi yao ya ufunguzi ya WAFCON Jumapili, lakini watapambana vikali ili kujikomboa katika mechi mbili zilizobaki. Starlets walipoteza 4-0 mikononi mwa wenyeji na lazima wawashinde Senegal na Algeria kwa njia ya kushawishi ili kupata nafasi yoyote ya kufuzu kwa nusu fainali. Timu nne bora katika mashindano hayo zitajikatia tikiti ya kombe la dunia la wanawake la 2027 nchini Brazil.
ODEMBA BELDINE - WAFCON
Malumbano yananukia katika soka ya Kenya baada ya vilabu vya NSL kutishia kususia kuanza kwa msimu wa mwaka 2026/27 isipokuwa FKF itapate mdhamini wa ligi. Wenyeviti wa vilabu vya NSL, wamekatishwa tamaa na shirikisho hilo kuzingatia ligi ya daraja la juu huku likiacha ligi ya daraja la pili nchini ikikabiliwa na matatizo. Wasiwasi huo unakuja huku vilabu viwili vikikaribia kuanguka na kubadilishana nafasi zao za ligi kutokana na matatizo ya kifedha. Msimu uliopita, mabingwa wa NSL hawakuwa na pesa zozote za zawadi ikilinganishwa na milioni 15 zilizoshindwa na mabingwa wa KPL.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Nairobi, Narok na Kajiado.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.