Chelsea wako kwenye mazungumzo ya kumsajili Jordan Henderson wa Brentford na Danny Welbeck wa Brighton. Kiungo wa kati wa Uingereza Henderson, mwenye umri wa miaka 36, amebakisha mwaka mmoja kwenye mkataba wake na Brentford lakini Bees wako tayari kumruhusu aondoke kwa uhamisho wa bure. Mshambuliaji wa zamani wa Uingereza Welbeck, wa miaka 35, ana hamu ya kuhamia Stamford Bridge na kuna matumaini kutoka kwa upande wa Chelsea kwamba makubaliano yanaweza kufikiwa. Welbeck ambaye alifunga mabao 13 ya ligi katika mechi 37 kwa Brighton msimu uliopita alitia saini nyongeza ya mkataba wa miezi 12 mwezi Machi.
Beki wa Uingereza John Stones yuko kwenye mazungumzo ya hali ya juu na Inter Milan kuhusu kujiunga na timu hiyo ya Italia kwa uhamisho wa bure. Beki huyo wa kati ni mchezaji huru baada ya kuondoka Manchester City mwishoni mwa Juni. Stones amekuwa akinyatiwa pakubwa kutoka kwa vilabu kote Ulaya, ikiwa ni pamoja na Chelsea na Juventus. Lakini Mabingwa wa Serie A Inter wamefanya mazungumzo mazuri na mchezaji huyo wa miaka 32 na inaeleweka kuwa anaongoza mbio za kumsajili kwa mkataba wa miaka miwili.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Eldoret, Kakamega na Kisumu.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.