Serikali inaboresha makaazi yasiyo rasmi katika kaunti 33 kupitia Mradi wa Uboreshaji wa Makaazi Yasiyo rasmi wa Kenya (KISIP), unaofadhiliwa kwa ushirikiano na Benki ya Dunia. Mpango huo unahusisha kuchora ramani za makaazi, kupima viwanja na kutoa hati miliki au barua za umiliki. Pia hutoa miundombinu muhimu, ikiwa ni pamoja na barabara, mifereji ya maji, taa za barabarani na mifumo ya usafi wa mazingira. Katibu wa Ardhi wa Kirinyaga Samuel Kanjobe anasema vijiji 148 vya kikoloni katika kaunti hiyo vinazingatiwa kwa ajili ya kuboreshwa.