Jaji Mkuu Martha Koome amezitaka taasisi za sekta ya haki kusonga mbele zaidi ya kupima mafanikio kupitia takwimu za kesi na badala yake kuzingatia kama Wakenya wa kawaida wanaweza kupata haki ambayo ni nafuu, inayoeleweka na inayokidhi mahitaji yao. Akiongea katika mkutano wa 38 wa Baraza la Kitaifa la Utawala wa Haki huko Mombasa, Koome alisema kipimo halisi cha mfumo wa haki kiko katika uzoefu wa wale wanaotafuta huduma zake badala ya idadi ya kesi zilizokamilishwa.
MARTHA KOOME - REFORMS