Serikali ya Kaunti ya Mombasa inaendelea na mchakato wa kutatua dhuluma za kihistoria za ardhi kupitia Ardhi Fund ambayo iliundwa ili kutatua tatizo la makaazi duni huko Mombasa. Katibu wa ardhi wa kaunti Mohamed Hussein alisema chini ya mpango huo, kaunti itanunua ardhi zenye mgogoro na kusaidia kuwapa makaazi maskwota kwa kutumia Ardhi Fund. Hussein, alisema Kaunti imejitolea kuhakikisha umiliki wa ardhi salama, mipango ya miji jumuishi, na suluhisho endelevu za makaazi.