Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe amewasihi wakulima wa chai kuunga mkono Ushuru wa Chai ulioanzishwa hivi karibuni, akisisitiza kwamba unalipwa na wanunuzi wa chai na sio na wakulima. Alieleza kwamba mapato kutoka kwa ushuru huo yatawekezwa tena katika sekta ya chai ili kufadhili utafiti, uuzaji wa kimataifa, mipango ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, uvumbuzi, na kuongeza thamani. Aliwasihi wakulima kupuuza taarifa potofu kuhusu ushuru huo.

MUTAHI KAGWE - AFFECT