Bidhaa bandia na zisizoidhinishwa za kudhibiti wadudu ziliunda chini ya asilimia moja katika soko la Kenya katika mwaka ulioishia Juni terehe 30, 2026, zikionyesha udhibiti mkali na hatua za sekta dhidi ya bidhaa haramu. Meneja mkuu wa Bodi ya Bidhaa za Kudhibiti Wadudu anayehusika na uzingatiaji sheria Lawrence Kalawa alisema ni tani nane tu za bidhaa haramu zilizorekodiwa, dhidi ya takriban tani elfu 22 za vifaa halali. Kalawa alisema hii inaashiria kupungua kwa hatari, huku sekta hiyo sasa ikipatia kipaumbele usimamizi wa bidhaa, elimu kwa wakulima, na udhibiti.
LAWRENCE KALAWA - BORDER