Seneta wa Nandi Samson Cherargei ameiomba NCIC kumchunguza kiongozi wa DCP Rigathi Gachagua kuhusu matamshi anayosema yanaweza kuwa ni upotoshaji wa kikabila na kudhoofisha mshikamano wa kitaifa nchini Kenya. Katika barua kwa Mwenyekiti wa NCIC, Cherargei alidai Gachagua alidai Rais William Ruto, Waziri wa Usalama na Naibu Insoekta Jenerali wa Polisi, wote kutoka jamii ya Kalenjin, waliunda kikosi maalum cha polisi kinachowalenga viongozi wa upinzani. Anaonya kauli hizo, zilizotolewa katika mikutano na mahojiano, zinahatarisha kuchochea mvutano wa kikabila na kudhoofisha amani.
SAMSON CHERARGEI - NCIC