Viongozi wa Jubilee wamelaani matamshi ya Waziri wa Afya Aden Duale, ambayo wanasema yanaonekana kuwalenga watu kutoka eneo la Mlima Kenya. Viongozi hao wakiongozwa na Jeremiah Kioni wanasema kwamba ni makosa kwa viongozi kuchochea jamii. Wanamtaka Waziri Duale ambaye ameitwa na NCIC kuomba msamaha hadharani.
JEREMIAH KIONI – DUALE