Wanafunzi saba kutoka Shule ya Kitaifa ya Wavulana ya St. Patrick's Iten katika Kaunti ya Elgeyo Marakwet wamezuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Iten baada ya kufikishwa mahakamani kwa madai ya kuchoma bweni la shule. Wakifika mbele ya Hakimu Mkuu Gladys Adhiambo, saba hao walishtakiwa kwa kuchoma bweni la shule hiyo Jumatano. Wanafunzi hao saba walikiri mashtaka hayo, na kesi hiyo imepangwa kutajwa Jumatatu wiki ijayo.