Wakaazi wa Isiolo wamehimizwa kushirikiana kwa karibu na mashirika ya usalama kwa kushiriki taarifa ambazo zinaweza kusaidia kupunguza uhalifu na kuimarisha usalama wa umma mjini humo. Akizungumza wakati wa mkutano wa usalama kufuatia mauaji ya mfanyabiashara mwanamke na washambuliaji wasiojulikana, Jumatatu jioni, Seneta wa Isiolo Fatuma Dullo, aliwataka wakaazi kutowalinda wahalifu, bali badala yake wawaripoti kwa siri kwa mamlaka husika. Alisema ushirikiano wa jamii na maafisa wa usalama na ujasusi ni muhimu katika kupambana na uhalifu.