Upatikanaji wa bima ya afya ya bei nafuu unatarajiwa kuimarika kote Afrika Mashariki baada ya Jubilee Health kushirikiana na kampuni ya kimataifa ya inurtech. Mkurugenzi Mtendaji wa Bima ya Afya ya Jubilee Njeri Njomo anasema ushirikiano huo utaunganisha bima ya afya katika majukwaa ya kidijitali ambayo tayari yanatumiwa na mamilioni ya watu, na kurahisisha wateja kununua na kusimamia bima. Kampuni hizo mbili zinasema mpango huo utapanua usambazaji wa bima, kupunguza vikwazo vya uandikishaji na kusaidia upatikanaji mpana wa huduma za afya kupitia suluhisho zinazoendeshwa na teknolojia.
NJERI NJOMO – PARTNERSHIP