Kiungo wa kati wa AC Milan, Luka Modric - ambaye anatimiza miaka 41 mwezi Septemba - ametia saini mkataba wa mwaka mmoja zaidi. Mkroatia huyo alijiunga na Milan msimu uliopita wa joto kwa mkataba wa mwaka mmoja na chaguo la kuongeza muda baada ya kuondoka Real Madrid. Baada ya miaka 13 huko Bernabeu, Modric ambaye alicheza Kombe lake la tano la Dunia akiwa na Croatia, alifunga mabao mawili katika mechi 37 akiwa na Milan katika msimu mmoja ambapo walimaliza wa tano katika Serie A na kufikia hatua ya 16 bora ya Coppa Italia.

Shirikisho la soka la Ujerumani litafanya mkutano na waandishi wa habari jioni ya leo huku Jürgen Klopp akitarajiwa kuwasilishwa kama kocha mpya wa timu ya taifa katika makao makuu yake ya Frankfurt. Meneja huyo wa zamani wa Liverpool amekuwa mgombea anayependelewa tangu Julian Nagelsmann ajiuzulu kufuatia kushindwa kwa Ujerumani kwa mikwaju ya penalti dhidi ya Paraguay katika raundi ya 32 ya Kombe la Dunia. Klopp ambaye amekuwa mkuu wa Soka la kimataifa wa Red Bull tangu mwaka 2025 hajafundisha, tangu aondoke Liverpool mwaka 2024 akidai kuwa na uchovu.

Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Kisumu, Eldoret na Kakamega.

Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.