Mswada wa Kura ya Maoni uko mbele ya Seneti huku wabunge wakiunga mkono juhudi za kuanzisha mfumo wa kisheria wa kuendesha kura ya maoni nchini. Seneta wa Bomet Hillary Sigei alisema maamuzi ya mahakama yamefichua mapengo katika sheria zilizopo, na kuacha nchi bila taratibu zilizo wazi za kuongoza kura ya maoni. Seneta wa Busia Okiya Omtatah aliunga mkono Muswada huo, akisema utatekeleza vifungu vya kikatiba na kutoa sheria zilizo wazi na zinazoweza kutekelezwa kwa kura za maoni zijazo.
OKIYA OMTATAH – BILL