Rais William Ruto amewasihi wanaume wa Kenya kukumbatia kupanga uzazi, akisema huduma za uzazi bila malipo chini ya mpango wa serikali wa Linda Jamii hazipaswi kuchukuliwa kama kisingizio cha kuwashinikiza wanawake kupata watoto zaidi. Akizungumza wakati wa mkutano na mafundi wa Kaunti ya Nairobi katika Ikulu, Ruto alisema serikali imepanua mpango wa zamani wa Linda Mama hadi Linda Jamii, kwa usaidizi ulioimarishwa kwa akina mama wajawazito kuanzia ujauzito hadi kujifungua.

WILLIAM RUTO – LINDA