Wanaume wawili waliokamatwa kwa madai ya kusafirisha Cocaine yenye thamani ya Sh milioni 3.9 watasalia kizuizini hadi tarehe 5 mwezi ujao, baada ya kukana mashtaka ya kula njama na ulanguzi wa dawa za kulevya. Hilton Chopeta na Mohamed Ali walifikishwa mbele ya mahakama ya Mombasa, ambapo Hakimu Mkaazi Mkuu David Odhiambo aliamuru ripoti ya kabla ya dhamana na kuamuru washukiwa waendelee kuzuiliwa.