Walimu wote wakuu wa shule za upili watahitajika kufika mbele ya Kamati ya Uwekezaji wa Umma ya Bunge ya Utawala na Elimu ili kujibu maswali ya ukaguzi Mwenyekiti wa kamati Dick Maungu amesema. Maungu, anasema hatua hiyo inalenga kuimarisha uwajibikaji na kupunguza usimamizi mbaya wa fedha za umma katika taasisi za elimu. Wakati huo huo, kamati ya uangalizi wa bunge imewaambia wakuu wa taasisi za elimu ya juu kuchukua mchakato wa ukaguzi kwa uzito, ikisema maafisa wa umma waliopewa pesa za walipa kodi lazima waonyeshe uwazi na usimamizi wa fedha kwa busara.