Wakuu wa Usalama nchini wamekaribisha idhini ya kimataifa ya Kitengo cha Usimamizi wa Uchunguzi wa Kisayansi na uzinduzi wa mfumo wa utambuzi wa kibiometriki, wakielezea maendeleo hayo kama hatua muhimu katika sekta ya polisi nchini Kenya. Wakiongozwa na mkurugenzi wa Uchunguzi wa Jinai Mohamed Amin walisema mipango hiyo itaimarisha taaluma, kuboresha usimamizi wa ushahidi na kuimarisha imani ya umma katika uchunguzi wa jinai.
VOX POP-LAUNCH