Imefichuliwa katika kesi ya mauaji ya marehemu Albert Ojwang kwamba picha za CCTV kutoka Hospitali ya Mbagathi ziliwanasa maafisa wa polisi wakimsafirisha kutoka Kituo Kikuu cha Polisi saa za asubuhi za tarehe 9 Juni, mwaka uliopita. Mkuu wa Uchunguzi wa Kisheria wa IPOA Joseph Mutua aliambia Mahakama Kuu ya Kibera kwamba picha hizo zilichunguzwa kwa njia ya kisayansi na kuthibitishwa kuwa halisi, bila dalili za kuharibiwa. Watu sita, akiwemo aliyekuwa OCS wa Kituo cha Polisi cha Central Samson Talaam, wanashtakiwa kwa mauaji ya Ojwang. Kesi hiyo itaendelea tena Desemba tarehe 14.

VOX POP – BODY