Kenya imepokea sehemu ya kwanza ya tani 4.5 za vifaa vya matibabu kutoka kwa serikali ya India ili kuimarisha utayari na mwitikio wa nchi dhidi ya dharura inayowezekana ya afya ya umma ya Ebola. Shehena hiyo ilikabidhiwa rasmi na Kamishna Mkuu wa India kwa Waziri wa Afya, Aden Duale, wakati wa sherehe iliyofanyika Jana. Mchango huo ni sehemu ya usaidizi mpana wa India kwa nchi za Afrika katika kuimarisha uwezo wao wa kuzuia na kukabiliana na mikurupuko ya Ebola.