Uongozi wa Kaunti ya Embu umejitetea vikali kuhusu shutuma za kutotekeleza miradi yoyote ya maendeleo inayoonekana na badala yake kudandia ile inayofanywa na Serikali ya Kitaifa. Naibu Gavana, Kinyua Mugo alisema kwamba imetekeleza miradi mikubwa ya maendeleo ya ugatuzi, huku ikishirikiana kimkakati na serikali ya Kitaifa ili kupata ufadhili kwa miradi mikubwa. Aliangazia miradi, kama vile uboreshaji unaoendelea wa barabara za mijini kote Kaunti hiyo kwa gharama ya Sh milioni 150.