Upinzani dhidi ya mapendekezo ya kugawanya eneo la Mlima Kenya kwa kambi za Mashariki na Magharibi unaendelea kuongezeka. Kiongozi wa Wengi katika Bunge la Kaunti ya Tharaka-Nithi Justin Kithinji amepuuza pendekezo hilo, ambalo limeungwa mkono na waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku, akisema linagawanya watu na linaendeshwa na maslahi ya ubinafsi. Amewasihi wakaazi katika eneo lote la Mlima Kenya kukataa hatua hiyo na badala yake waendelee kuwa wamoja.
JUSTIN KITHINJI – OPPOSE