Benchi la ufundi na usimamizi wa Gor Mahia kwa pamoja limemchagua Sylvester Owino kama nahodha, baada ya kustaafu kwa Philemon Otieno. Rais wa klabu hiyo Ambrose Rachier unasema uongozi, taaluma na utendaji wa Owino ulimpa wadhfa huo. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Kenya atasaidiwa na beki Mike Kibwage na Alpha Onyango. Otieno alihudumu KO’gallo kwa miaka 10 na anachukua rasmi wadhifa wa meneja wa timu huku KO’gallo wakianza kampeni yao ya CECAFA dhidi ya wenyeji APR FC katika Uwanja wa Amahoro jijini Kigali Rwanda Ijumaa.
Shabana FC imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa zamani wa Kenya U20 Luis Ingavi, ambaye anarejea Kenya baada ya kukaa miaka kadhaa nchini Marekani. Mshambuliaji huyo aliyepewa sifa kubwa anajiunga na timu hiyo ya Gusii baada ya kupata uzoefu muhimu nchini Marekani, ambapo alichezea Midwest United katika Ligi ya Pili ya USL na Chuo Kikuu cha Valley State. Nahodha huyo wa zamani wa Goseta Boys alihamia Marekani kupitia ufadhili wa masomo katika Chuo cha Montverde huko Florida. Kuwasili kwake kunaimarisha safu ya mashambulizi ya Shabana kabla ya msimu mpya wa Ligi Kuu ya FKF.
Vipindi vya anga kavu vinashuhudiwa Eldoret, Kisumu na Kakamega.
Ili kupata habari zaidi tembelea tovuti ya radiojambo.