Serikali imewaonya waajiri na kampuni zilizopewa kandarasi kwa miradi ya umma dhidi ya kuchelewesha mishahara ya wafanyakazi. Waziri wa leba Alfred Mutua alisema hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya mwanakandarasi anayejenga Talanta Sports City kwa madai ya kushindwa kufuata sheria za kazi kufuatia kifo cha mfanyakazi Sammy Kyego. Mwili wake ulipatikana katika eneo hilo, huku familia yake ikisema hapo awali alikuwa ameelezea kukerwa kwake na kucheleweshwa kwa mishahara.


ALFRED MUTUA-SUE