Seneti imekataa ombi la kutaka kuanzishwa kwa mfumo wa kisheria unaowaruhusu Wakenya kumwondoa Rais na magavana kabla ya mwisho wa muhula wao. Ombi hilo, lililowasilishwa na mwanaharakati Laban Omusundi wa Nakuru, lilitupiliwa mbali baada ya Kamati ya Haki, Masuala ya Kisheria na Haki za binadamu ya Seneti kugundua kuwa Bunge halina mamlaka ya kikatiba ya kutunga sheria kama hiyo. Kamati hiyo ilisema pendekezo hilo linakinzana na Katiba, ambayo tayari inatoa taratibu maalum za kuondolewa kwa Rais na magavana.


VOX POP – VOTE