Rais William Ruto amewapa changamoto viongozi aliowashutumu kwa kukosa ari na dhamira ya kubadilisha nchi, watoke kwenye jukwaa la kisiasa. Ruto alisema wale ambao wamepoteza nguvu ya kutekeleza wanapaswa kujiondoa badala ya kuizuia Kenya. Alisema maendeleo ya Kenya yanategemea viongozi wanaoamini katika uwezo wa nchi hii na wako tayari kusukuma mageuzi licha ya changamoto.
WILLIAM RUTO - CHALLENGE