Waziri wa Mambo ya Ndani KipchumbaMurkomen ameitaka Mahakama kutoa adhabu kali zaidi kwa watu waliohukumiwa kwa ujambazi, akisema adhabu kali itazuia matumizi ya magenge ya kukodi ili kuchochea vurugu. Alibainisha kuwa vyombo vya usalama vimefanikiwa kudhibiti vitisho tata na bado vina uwezo wa kushughulikia shughuli za ujambazi zinazoendeshwa na kisiasa kote nchini. KIPCHUMBA MURKOMEN - HAIWEZEKANI