Kamati ya Usalama ya Kaunti ya Nyandarua imewaonya wananchi dhidi ya majaribio ya kubaki katika vituo vya kupigia kura kwa kisingizio cha "kulinda kura," wakisisitiza kwamba jukumu la kulinda mchakato wa uchaguzi liko kwa mawakala wa usalama na IEBC pekee. Kamishna wa Kaunti Abdirisack Jaldesa alisema mipango ya kutosha ya usalama imewekwa ili kuhakikisha uchaguzi mdogo wa bunge la Ol Kalou wa amani, huru na unaoaminika.


ABDIRISACK JALDESA – USALAMA