VIJANA wawili wenye umri wa makamo wamekamatwa na makachero wa DCI baada ya kudaiwa kumuibia mteja wao takribani shilingi laki tatu.
Kwa mujibu wa ripoti ya DCI, vijana hao walijifanya warembo wa kutoa huduma za kukanda watu miili kabla ya kumwimbia mtu mmoja ambaye alikuwa mteja wao shilingi 280,000.
“Washukiwa hao wamekuwa wakiwarubuni wateja wasiotarajia kwa kutangaza “huduma za kitaalamu za masaji” mtandaoni. Lakini badala ya massage ya kufurahi, waathirika hukutana na mshangao usiovutia,” sehemu ya simulizi ya DCI ilisema.
Wawili hao walisemekana kuwa na nyumba ya kutoa huduma ya masaji katika mtaa wa Lumumba mtaani Kasarani ambapo wamekuwa wakiwarubuni wateja na kisha kuiba vitu vyao.
Siku yao ya 40 ilifika pale walipomrubuni mmoja na baada ya kumfikisha kwenye nyumba, badala ya kumhudumia kwa masaji, walichomoa visu na kumtaka kusalimisha kila kitu.
“Kwa kulazimishwa, mwathiriwa alilazimika kuhamisha Sh280,000 kwa nambari ya simu ya washukiwa, na kuporwa vitu vyake vya thamani kabla ya kutupwa nje isivyo halali.”
“Uchunguzi ulianzishwa, na kupitia wapelelezi wa kitaalamu, wawili hao walitiwa mbaroni walipokuwa wakiburudika katika eneo la gereza la Kamiti, pengine wakitumia pesa zilizoibwa,” DCI walifichua.
Wawili hao kwa sasa wako chini ya ulinzi, wakiendelea na mchakato wa kufikishwa mahakamani.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!