Museveni

MWANAMUME mwenye umri wa makamo ambaye mwezi jana alizuiliwa na walinzi wa rais Yoweri Museveni wa Uganda akijaribu kumkimbilia rais huyo amekiri makosa yake.

Kijana huyo alionekana kuwa na nia ya kumfikia rais Museveni wakati wa mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Kawempe Kaskazini lakini kwa bahati nzuri akazuiliwa na walinda usalama wa rais.

Kulingana na jarida la Daily Monitor, Yoram Baguma, 28, sasa amekiri mashtaka yake ya kutaka kumshambulia na kumdhuru rais na kuomba msamaha.

‘Ningependa kuomba radhi kwa shtaka la kujaribu kumshambulia rais,” Baguma ambaye alikuwa anazungumza kwa lugha ya Runyankore alisema kupitia kwa mtafsiri wa mahakama.

Jamaa huyo alisomewa mashtaka kwamba mnamo Machi 11 wakati wa siku ya mwisho ya kampeni za uchaguzi mdogo wa Eneobunge la Kawempe North katika uwanja wa Mbogo, alikiuka maagizo ya kiusalama na kuonyesha nia ya kumdhuru, kumshambulia na kumkera rais.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika video ambayo ilisambazwa mitandaoni, Baguma alionekana kwenye kasi ya ajabu kuelekea kwa rais Museveni lakini kabla ya kumfikia, aliweza kuzuiliwa na walinda usalama.

Museveni alikuwa anafanya kampeni kwa mgombea wa chama tawala cha NRM, Faridah Nambi ambaye hata hivyo aliibuka wa pili baada ya kushindwa na mgombea wa chama cha upinzani cha NUP, Elias Nalukoola.

Baada ya kukiri mashtaka yake, Baguma alirudishwa rumande baada ya hakimu kuahirisha kesi hiyo hadi Mei 30, wakati ambapo Baguma atakuwa amepata wakili kwani kesi inayomkabili inavutia hukumu ya pili kwa ukubwa nchini Uganda.