
WAFANYIBIASHARA katika mji mkuu wa kaunti ya Kiambu, Thika wamejitokeza kulalamika kwa kile wanadai wanawake wa kujiuza kimwili wamefurika na kuvuruga biashara zao.
Wakizungumza na K24, wafanyibiashara hao walisema kwamba katika siku za hivi karibuni, wasichana wengi katika umri wa miaka 14-15 wamejaa kujiuza kimwili na kuwavuruga wateja wa biashara zao.
“Kile kitu kimenishangaza ni kwamba hii biashara yao imezidi, hata tunaona wasichana wengine wadogo, akikataa shule anaingia kwa hiyo biashara. Ukija hapa jioni, sijui kama ni wa umri wa miaka 14 ama 15 ndio wamejaa hapa,” alilalamika mfanyibiashara mmoja.
Walisema kwamba wachuuzi hao wa tunda haramu wamejaa kiasi kwamba wameanza kuzua usumbufu kwa kila mwanamume anayepita hivyo kuwafanya wanaume kuogopa kuingia katika soko hilo na hivyo kuwafungia riziki zao za biashara halali.
“Ni vizuri serikali kuchukua hiyo hatua ya kukomesha hayo mambo ili hata wale wako nyumbani wadogo wasikuwe eti wakipotea shule wanakuja hapa.”
Mmoja alisema kwamba wasichana hao wanakuja na kujianika mbele ya biashara zao hivyo kuwazuia wateja wao dhidi ya kufikia maduka yao.
“Hiyo huwa inakera sana maana wanakuja hapa mbele ya biashara zetu wanasimama huku. Unapata hata mteja anashindwa kuingia huku,” alisema.
Wengine walilalamika kwamba wasichana hao wamefikia hatua ya kuita na kukonyezea hata wanaume wanaopita hapo na wake zao bila kuwa na hata ncha ya heshima.
Tazama malalamishi yao hapa:
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!