Yoweri Museveni, rais wa Uganda

RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni ameonekana kughadhabishwa na utafiti mpya unaofanywa na watafiti katika chuo kikuu cha Makerere ambao wanafumbua njia mpya ya kuongeza lishe ya nyama na Samaki kwenye vyakula vya ng’ombe.

Wakati wa uzinduzi wa Wiki ya Utafiti na Ubunifu mwaka huu katika chuo hicho kikuu, Museveni alitambulishwa kwa mradi unaohusisha samaki na nyama kwenye chakula cha ng'ombe.

Rais huyo ambaye ni mfugaji wa ng’ombe wengi alikuwa wa haraka kuonyesha mashaka yake katika utafiti huo, akisema kwamba unapotosha kutoka tamaduni za tangu jadi za kulisha ng’ombe nyasi na majani tu.

“Nimeona tu kwenye vibanda watu wanatengeneza vyakula vya mifugo. Niliona kwamba wanawafanya ng'ombe kula samaki ... kwamba malisho ya ng'ombe yana samaki na nyama.”

Kulingana na Museveni, ni vizuri ng’ombe kusalia katika kulishwa nyasi na majani tu kwa sababu Samadi yao hutumiwa katika kuboma nyumba za matope na ikifikia wanalishwa nyama kama binadamu, basi kinyesi chao kitakuwa kinanuka kisiweze kutumika tena katika shughuli kama hizo na binadamu.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Katika Ankole, kinyesi cha binadamu kina jina, na kinanuka sana kwa sababu ya kile ambacho wanadamu hula. Tunakula nafaka, nyama n.k. Ng'ombe, kwa upande mwingine, wana jina la kinyesi chao, ambacho hakina harufu; hata tunaishughulikia na kuitumia kupamba nyumba zetu. “

“Lakini sasa naanza kuwa na wasiwasi. Ikiwa ng'ombe anakula chakula cha binadamu, bado hutoa kinyesi chake cha asili?” Museveni alihoji.

Alihoji zaidi ikiwa mfumo wa mmeng'enyo wa ng'ombe, ambao ni wanyama wanaokula mimea, unaweza hata kushughulikia lishe kama hiyo.

“Kuku na nguruwe wanaweza kulishwa kwa nyama kwa sababu hata kwa asili wanaweza kuishughulikia, lakini ng'ombe, mbuzi na kondoo, tunahitaji kutafuta njia zingine ambazo hazihusishi kuwalisha kwa nyama.”

Rais alipendekeza kuwa ingawa sayansi inaweza kutoa fursa mpya, baadhi ya mazoea yanapaswa kuchukuliwa kuwa "mwiko" na kukataliwa, haswa wakati yanatatiza mifumo asilia.