
SENETA wa Kakamega, Boni Khalwale amevutia maoni kinzani kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuongoza zoezi la uzinduzi wa choo katika ustani ya Muliro.
Kupitia ukurasa wake wa X, Khalwale alidai kwamba alilazimika kuzindua choo hicho baada ya kupata uvumi kwamba gavana Fernandes Barasa alikuwa na njama ya kutumia bustani hiyo kwa manufaa binafsi.
“Nilipatia gavana onyo Jumamosi ya kwamba nitakuja hapa leo [Jumatatu] asubuhi kufungua choo. Na nikampa nafasi kwamba kako ako na nguvu nyingine ambayo imeshinda Katiba ya Kenya aje tukutane naye hapa mimi nikifungua choo na yeye anizuie kufungua choo halafu tuone ni nani atahabatika kufaulu,” Khalwale alisema.
Akitetea hatua yake ya kufika kuzindua ufunguzi wa choo, Khalwale alisema kwamba yeye ni mwananchi mfuata sheria na hakuenda kuongoza zoezi hilo kwa maringo.
“Mimi ni mwananchi anayefuata sheria na siwezi kuja hapa kwa maringo kwa hivyo nilikuwa nimetuma wenye wamesimamia hii choo katika mahakama ambayo ilitoa kibali kwamba hii choo inastahili kufunguliwa,” aliongeza.
Alidai kwamba gavana Barasa alielekea katika mahakama ya rufaa kutaka hati ya kusimamishwa kwa shughuli ya ufunguzi wa hicho choo lakini mahakama ikasema ni jambo la dharura hivyo kumtaka yeye kukizindua.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!