Jeshi la Mynamar

BBC Burma imethibitisha kuwa watu saba waliuawa katika shambulio angani huko Naungcho, kaskazini mwa jimbo la Shan, chini ya saa tatu baada ya tetemeko hilo kutokea siku ya Ijumaa..

Makundi ya waasi wanaounga mkono demokrasia ambayo yanapambana kuwaondoa wanajeshi madarakani pia yameripoti mashambulizi ya angani katika kitongoji cha Chang-U katika eneo la kaskazini-magharibi la Sagaing, kitovu cha tetemeko hilo.

Pia kuna ripoti za mashambulizi ya anga katika mikoa iliyo karibu na mpaka wa Thailand.

Mtaalamu Maalum wa Umoja wa Mataifa Tom Andrews aliambia BBC siku ya Jumamosi kwamba "ni jambo la kushangaza" kwamba jeshi linaendelea "kurusha mabomu wakati tunajaribu kuokoa watu" baada ya tetemeko la ardhi.

Jeshi hilo ambalo limekuwa likishindwa mara kwa mara na la kufedhehesha na kupoteza maeneo mengi, limekuwa likitegemea zaidi mashambulizi ya anga ili kukandamiza upinzani dhidi ya utawala wake.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans