Ugali

WAKAAZI wa kijiji cha Kilimani kaunti ya Kakamega waligubikwa na butwaa kufuatia mkasa wa mauaji ya kifamilia.

Kwa mujibu wa ripoti, vijana wawili ambao ni kaka wa toka-nitoke walizozania kiasi cha ugali ambacho wangepika kupelekea mmoja wao kuuawa na mwenzake.

Reuebn Lutaboni mwenye umri wa miaka 42 alizozana na kakake mdogo Michael Lukala mwenye miaka 40 kuhusu kiasi cha ugali ambacho wangestahili kupika wakati Lutaboni alimshambulia mwenzake na kumuua.

“Wawili hawa walikuwa ni marafiki ambao wangefanya vibarua kijijini na walirudi nyumbani kupika chajio wakati mzozo ulipotokea. Mmoja alikuwa anapika wakati mwenzake alimshambulia na shoka kichwani mara kadhaa. Alimgonga kwa ubongo karibu mara 5, upande wa macho akamgonga mara 3 halafu upande wa macho akakata kabisa na kummaliza,” ndugu mkubwa alisema.

Cleophas Barasa, mzee katika kijiji hicho alilaani kitendo hicho huku akitoa wito kwa watu kutatua tofauti zao kwa njia zifaazo kuliko vita.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Mambo kama haya ya chakula haistahili ndugu kupigana mpaka mwingine anaua mwenzake kwa sababu ya chakula. Watu ambao wako zaidi ya umri wa 40 kuishi pamoja pia ni hatari kwa sababu hujui ni nini kitatokea baadae,” mzee huyo alishauri.