Mzee Victor Ombisi Sikote wa Embwali, Vihiga arudi nyumbani baada ya kutoweka kwa miaka 70

MBWEMBWE na nderemo zilishuhudiwa katika kijiji cha Embwali katika kaunti ya Vihiga baada ya mzee mmoja aliyetoweka nyumbani kwa miaka 70 kurudi akiwa hai.


Ombisi Sikote, mwenye umri wa miaka 92 sasa aliondoka nyumbani akiwa na miaka 22 akidai anakwenda kutafuta ajira katika kaunti ya Kiambu mnamo 1955.


Baada ya kuondoka nyumbani, mzee Sikote hakuweza kurudi nyumbani tena na juhudi za kumtafuta ziligonga mwamba baada ya familia kutowasiliana naye kwa zaidi ya miaka 60.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans


Hata hivyo, kijiji hicho kilishuhudia jambo la kustaajabisha mzee huyo aliporudi nyumbani akiwa kwenye kiti cha magurudumu.


“Kama wiki mbili zilizopita tulipata fununu kuhusu alikotoka, na hiki kikundi kikanituma hapa nikakuja na tukakaa pamoja na jamii na uongozi wa eneo hili na wazee wa kijiji wakamkubali huyu mzee,” mmoja wa waliomrudisha nyumbani aliambia runinga ya Citizen.

×

Suala la wazee kurudi katika familia zao baada ya kutweka kwa miongo kadhaa si geni nchini.


Mwezi Oktoba mwaka jana, familia moja kutoka kaunti ya Kisii ilimpokea mzee wao mwenye umri wa miaka 70 ambaye alipotelea kaunti ya Baringo kwa zaidi ya miaka 34.


Aidha, kisa sawia kilitokea nchini Uganda mwaka 2023 wakati mzee mwenye umri wa miaka 111 aliyetoka nyumbani akiwa na miaka 44 kurudi nyumbani baada ya miaka 66.


Mwaka wa 2020, mzee Joseph Chepwony alikaribishwa nyumbani kwake katika kaunti ya Elgeyo Marakwet baada ya kutoweka kwa miaka 45.