Raila Odinga na Kalonzo Musyoka

KINARA wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka ameendeleza harakati zake za kumshambulia spika wa Bunge la kitaifa kwa kile anadai kwamba anahujumu haki ya Kidemokrasia ya kutotambua muungano wa Azimio kama wa walio wengi bungeni.

Akizungumza mapema Jumatano, Musyoka alisema kwamba spika Moses Wetang’ula ni rafiki yake lakini wanaenda kumchukulia hatua za kisheria kwa kutoheshimu uamuzi wa mahakama.

Spika huyo anatarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu ni nani wanafaa kuketi upande wa walio wengi na wachache katika bunge la kitaifa baada ya mkanganyiko kushuhudiwa bungeni Jumanne katika kikao cha kwanza mwaka huu.

Musyoka pia alisema kwamba mapambano dhidi ya utawala wa rais Ruto yataendelea huku akimtaka Raila Odinga iwapo atafeli kupata wadhifa wa AUC arudishe nguvu zake katika harakati za kuikosoa serikali humu nchini.

“Hiyo vita inaendelea kwa bunge itaendelea. Ule wizi waliibia Raila mahakama imeonyesha wazi kwamba wabunge wengi ni wa Azimio. Spika anajaribu kujitetea na mahakama imesema huwezi. Huyu spika ni rafiki yangu lakini anaenda kuitwa kwa kudharau mahakama,” Musyoka alisema.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

“Raila anaenda kutafuta kiti AU, namwambia aende lakini akiona kimeumana arudi hapa tukomboe nchi ya Kenya,” Kalonzo aliongeza.

Siasa za ni mrengo upi ulio na uwakilishi mwingi bungeni zimeshamiri nchini tangu mwishoni mwa wiki jana mahakama ilipoamua kesi iliyowasilishwa kuhusu suala hilo.

Kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama, muungano wa Azimio la Umoja One Kenya ulikuwa na wawakilishi wengi kwenye mabunge yote mawili.

Hata hivyo, Septemba 2022 spika wa bunge Moses Wetang’ula aliamuru kwamba UDA kilikuwa na uwakilishi mwingi na hivyo kukabidhiwa nyadhifa za walio wengi bungeni.