Kenya yatambua watu wa jinsia ya huntha

NI ushindi mkubwa na wa kipekee kwa watu wenye jinsia mseto nchini baada ya serikali kutambua rasmi kwenye gazeti la serikali watu wa maumbile hayo.

Notisi ya Gazeti rasmi la serikali ya mwaka huu 2025, imetambua rasmi jinsia mseto kama jinsia ya tatu na sasa watoto wanaozaliwa na jinsia mseto wana kila haki ya kutambuliwa hivyo kwenye vyeti vya kuzaliwa.

Katika Sensa ya 2019, takribani watu 1,524 wa jinsia mseto walirekodiwa, ambayo ni asilimia 0.003 ya idadi ya watu nchini lakini idadi kamili haijulikani kwa sababu hakuna mfumo rasmi wa kukusanya data juu ya watu wa jinsia hiyo.

Utambulisho huu ni ushindi mkubwa wa haki ya kimsingi ya watu wa jinsia mseto ambayo imekuwa ikipiganiwa na mashirika mbalimbali ya kutetea haki za kibinadamu kwa muda mrefu.

Awali, tume ya kitaifa ya haki za kibinadamu nchini KNHCR iliarifu kwamba huenda idadi kamili ya watu wenye jinsia mseto ni zaidi ya 1.4m nchini Kenya.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Maombi ya kazi pia yalikuwa magumu, kwani hayaanguki ndani ya jinsia mbili zinazojulikana za wanawake na wanaume.

Huntha si jambo geni. Imekuwapo kwa muda mrefu kama wanadamu wamekuwepo.

Miongoni mwa majina ya zamani zaidi ya jinsia tofauti ni katika Biblia Takatifu, katika kitabu cha Mathayo katika Agano Jipya.

Biblia inakiri kuwepo kwa matowashi kwa kuzaliwa, matowashi ambao wamefanywa hivyo na wengine na matowashi ambao wamechagua kudhabihu anasa za kilimwengu kwa ajili ya Ufalme wa Mungu.