
MWANAMKE mmoja alikamatwa baada ya kudaiwa kumkata mume wake uume wake kwa sababu hakuweza kusisimka wakati wa kujamiiana.
Mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 48 aliwaambia polisi kuwa alimkata mume huyo mwenye umri wa miaka 58 baada ya kukosa kusisimka walipokuwa wakifanya mapenzi nyumbani kwao Jumapili.
Tukio hilo liliripotiwa kwa polisi wa Rondonia, nchini Brazili wikendi iliyopita ambapo mshukiwa mwenyewe aliandikisha ripoti kwamba yeye na mume wake walikuwa wamekunywa alasiri kabla ya kukata uanaume wake.
Baada ya kuona kwamba hakuwa na uwezo wa kusisimka, mwanamke huyo alienda jikoni kwao na kuchukua kisu kikubwa na kumkata kiungo chake.
Mwanamume huyo alikimbia nje ya nyumba yake na kutapatapa katika mtaa mzima.
Wawili hao walivamia makazi ya jirani kabla ya Idara ya Zimamoto ya Rondônia kufika. Wahudumu wa afya walimkimbiza katika hospitali ya eneo la Cacoal, ambako alitibiwa, chanzo kilisema.
Mwanamke huyo aliwekwa kizuizini kabla ya kesi kama sehemu ya uchunguzi.
Hii si mara ya kwanza kwa visa vya wake kuwashambulia wanaume wao katika ndoa na kutaka viungo vyao vya kiume katika taifa hilo la Amerika Kusini.
Mwezi Mei, mahakama katika mji wa kusini-mashariki wa Brazili wa Atibaia ilimhukumu Daine dos Santos kifungo cha miaka minne na miezi minane jela kwa kukata uume wa mume wake mwenye umri wa miaka 39, Gilberto de Oliveira.
Mama huyo wa watoto watatu mwenye umri wa miaka 34, ambaye ana mtoto wa kike na de Oliveira, alikuwa anakabiliwa na kifungo cha hadi miaka 30 jela kwa kosa la kujaribu kuua.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!