
RAIS William Ruto amewatolea pofu baadhi ya wanasiasa na wakenya wanaojaribu kukosoa sera zake.
Akizungumza katika kaunti ya Garissa wakati wa ziara yake ya kimaendeleo katika eneo pana na Kaskazini Mashariki, kiongozi wa taifa alisema kwamba yeye sit u kiongozi lakini pia ni msomi mwenye kitembo cha PhD.
Rais alisema kwamba baadhi ya watu wanaojaribu kukosoa sera zake haswa mpango wa chanjo kwa mifugo ni wa elimu kidogo ambao hawana nafasi ya kumshauri wala kumfundisha.
“Na mkiona wale wanalalamika sijui wamesomea wapi. Si mimi niko na PhD? Si mimi naenewa nini inaendelea Kenya? Sasa mimi Napata watu wengine wako na elimu kidogo kidogo wanajaribu kunifundisha, mnanifundisha kazi gani?” rais alisema.
Kiongozi huyo aliwarai watu kutoka jamii za wafugaji katika kaunti ya Garissa kutopinga mifugo wao kudungwa chanjo.
Kwa mujibu wa rais Ruto, Garissa ni kaunti ya pili kwa wingi wa mifugo baada ya Turkana akisema kwamba wafugaji hao watanufaika na chanjo ya bure ambayo inatolewa na serikali yake.
“Hii Garissa ndio kaunti yenye iko na ng’ombe nyingi sana Kenya. Kenya hii ni ya 3 kwa wingi wa mifugo barani Afrika n akaunti ambayo inaongoza ni Turkana ikifuatwa na hii ya Garissa….na ndio sababu hiyo nimesema ile pesa mmekuwa mkitumia kwa chanjo ya ng’ombe sasa serikali ya Kenya itawalipia.”
“Kama tunataka kuendesha ukulima ili nyama yetu iwe na bei ya sawasawa, na maziwa yetu yauzwe katika masoko ya Kenya na nje ya nchi, lazima tuwe taifa lililo huru kutokana na magonjwa. Kama tuko na magonjwa kwa mifugo wetu tutakuwa wenyewe tunakwaza ile soko ambayo tungepata kwa ajili ya mifugo yetu,” aliongeza.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!