Fisi

WANASAYANSI walipigwa na butwaa kufuatia kuripotiwa kuonekana kwa fisi mwenye madoadoa kusini mashariki mwa Misri, ambayo inasemekana kuwa ni mara ya kwanza kukutana na mnyama huyo nchini humo katika takriban miaka 5,000.

Kwa mujibu wa chombo cha habari nchini humo – Mamalia, Fisi huyo alionekana na wenyeji wa Wadi Yahmib, karibu maili 19 kutoka mpaka wa Misri na Sudan, ambao walimkamata na kumuua mnyama huyo.

Kulingana na jarida la Mammalia, ambalo hufanya hesabu, uchambuzi, na tafsiri ya anuwai ya wanyama jamii ya mamalia, fisi alionekana mnamo Februari 2024, lakini ripoti hiyo sasa inachunguzwa zaidi.

Mwanaikolojia wa Misri Abdullah Nagy, ambaye anafanya kazi katika Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini humo, aliwaambia waandishi wa habari wiki hii "maoni yake ya kwanza yalikuwa kutoamini hadi nilipoangalia picha na video za mabaki".

"Nilishangazwa kabisa. Ilikuwa zaidi ya chochote tulichotarajia kupata huko Misri," aliendelea.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Mnyama huyo ana asili ya Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara na anajulikana kuwa na uwezo wa kusafiri hadi maili 17 kwa siku.

Kulingana na Mammalia, fisi wenye madoadoa "wanaweza kubadilika kwa urahisi, wanaishi katika anuwai ya makazi.”

Makazi yao ya asili ni mchanganyiko wa msitu-savanna, lakini pia inaweza kupatikana katika jangwa na misitu.

Ugunduzi huo umewafanya watafiti kutafakari iwapo tukio hilo limetokana na hali ya hewa isiyo ya kawaida ambayo imefungua njia ya uhamiaji, na kuruhusu fisi mwenye madoadoa kusafiri zaidi ya maeneo yake ya kawaida ya uwindaji.

Mzunguko wa hali ya hewa ya asili ni sehemu ya Njia ya Bahari Nyekundu, eneo la shinikizo la chini ambalo linakabiliwa na mvua kali na mafuriko, pamoja na upepo mkali.

Mzunguko wa hali ya hewa hutokea karibu mara moja kwa muongo mmoja lakini hivi karibuni umesababisha mvua zaidi katika eneo la mpaka wa Misri na Sudan.

Watafiti wanaamini kuwa hali ya hewa huenda iliongeza ukuaji wa mimea na kupelekea fisi hao kutengeneza njia ya uhamiaji wakati wa kutafuta wanyama wa kuwinda.

Ripoti mbalimbali zinasema kwamba picha za satelaiti zilifichua viwango vya ongezeko la ukuaji wa mimea katika miaka mitano iliyopita katika eneo hili, na kuunga mkono nadharia hizo.