
Chanzo cha picha,EPA
Nchi zinazoongozwa na jeshi Mali, Niger, na Burkina Faso zimejiondoa rasmi katika Jumuiya ya Uchumi ya Mataifa ya Afrika Magharibi (ECOWAS), na kusababisha mgawanyiko katika muungano huo wa Afrika Magharibi.
Nchi hizo tatu ziliunda muungano wake unaojulikana kama Alliance of Sahel States (AES), baada ya Ecowas kushutumu mapinduzi ya kijeshi, na kusimamisha ushirika wao, kwa matumaini ya kurejesha utawala wa demokrasia.
Maelfu ya watu walikusanyika katika nchi za Niger, Burkina Faso na Mali siku ya Jumanne kuunga mkono kujiondoa kutoka kwa muungano wa eneo ambako kunaanza rasmi Jumatano.
Hatua hii inafuatia ilani iliyomalizika muda wake ambayo ni lazima kutolewa ya mwaka mmoja.
Nchi hizo tatu zilikosoa ECOWAS kwa vikwazo ilivyowawekea baada ya mapinduzi na sasa zinapanga kuunda jeshi la umoja na kukuza uchumi kupitia muungano mpya wa maeneo ya Sahel.
Kujiondoa kwao kutoka kwa muungano huo kunaonekana kudhoofisha umoja wa kikanda na ushirikiano wa usalama katika kupambana na makundi ya kigaidi.
Na tangu wakati huo, nchi hizo tatu zimekata uhusiano na Ufaransa, ambayo ndio koloni yao na kuanzisha ushirikiano mpya na Urusi.
Ecowas inasema maeneo ya Sahel yana kipindi cha miezi sita kutoka tarehe ya mwisho ya Jumatano kujiunga tena na muungano huo ikiwa wataamua kufanya hivyo.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!