KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Alhamisi Novemba 28.
Katika taarifa ya siku ya Jumatano jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti nne za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na Nairobi, Homa Bay, Nyeri, na Kiambu.
Katika kaunti ya Nairobi, eneo la AA litaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Maeneo ya Kanyadhiang na Nyakwere katika kaunti ya Homabay pia yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi alasiri.
Eneo la Kamwenja TTC katika kaunti ya Nyeri litaathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Sehemu za maeneo ya St Julian's, Terrasol, Wangige, na Kingeero katika kaunti ya Kiambu pia yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!