KAMPUNI ya kusambaza umeme nchini Kenya (KPLC) imeonya kuhusu kukatizwa kwa umeme katika maeneo kadhaa nchini siku ya Jumatano, Novemba 27.

Katika taarifa ya siku ya Jumanne jioni, kampuni hiyo ilitangaza kwamba baadhi ya maeneo ya kaunti saba za Kenya yatakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Kaunti ambazo zitaathirika na kukatizwa kwa umeme ni pamoja na  Nairobi, Kajiado, Bomet, Narok, Kakamega, Nyeri, na Murang'a.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu za maeneo ya Kasarani, na Kaloleni Jogoo Road zitaathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Sehemu za mji wa Ngong katika kaunti ya Kajiado zitakosa umeme kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Enjoying this article? Subscribe for unlimited access to premium sports coverage.
View Plans

Katika kaunti za Bomet na Narok, maeneo ya Mulot, Sachora na Baraka yataathirika kati ya saa mbili asubuhi na saa kumi unusu alasiri.

Maeneo ya hospitali ya Iguhu na Khaega katika kaunti ya Kakamega yataathirika na kukatizwa kwa umeme kati ya saa tatu unusu asubuhi na saa kumi na moja jioni.

Katika eneo la Mt Kenya, maeneo ya Mathioya, Mioro, Nairutia na Marina yataathirika kati ya saa tatu asubuhi na saa na moja jioni.