
Aliyekuwa naibu wa rais, Rigathi Gachagua amefichua
kwamba maisha yake yamekuwa yakiendelea kwa njia nzuri tangu kubanduliwa kwake.
Akipuuzilia mbali uwezekano owote wa kuzama kwenye
bahari ya mawazo baada ya kupoteza kazi yake kama naibu wa rais, Gachagua
alisema kwamba kwa sasa yeye yuko vizuri kabisa, akiwashukuru Wakenya kwa
kumuombea.
Mwanasiasa huyo alikuwa anazungumza JUmapili katika
ibada kaunti ya Kajiado ambapo alisema hata yeye ni kama rais mstaafu Uhuru Kenyatta
ambaye alisema Jumamosi kwamba hana mambo mengi kwani anaangalia runinga na
kusikiliza redio kama Wakenya wengine tu.
“Mimi
sina maneno mengi, yangu tu ni kusema ahsante sana. Ningependa kuwashukuru watu
wa Kajiado ya Kaskazini kwa maombi yenu. Na mimi sina stress, mimi nime’relax
vizuri sana. Sasa hakuna mtu ananilaumu kwa ile shida iko Kenya, wengine
walaumiwe, wajibu,” Gachagua alisema.
“Mimi
ni mtu sasa wa kuangalia. Hata Uhuru Kenyatta, rais wetu alisema yeye yake ni
kuangalia kwa TV na kusikiliza kwa redio. Hata mimi naangalia Tv na kusikiliza
redio. Wacha wale wanaendesha walaumiwe,” Gachagua
aliongeza.
Kiongozi huyo hata hivyo aliwarai wananchi
kuwaheshimu viongozi wao, akilenga mkuki kwa serikali ya Ruto kwamba kama yeye
ndiye alikuwa shida sasa shida inafaa kuwa imeisha baada ya kumbandua.
“Acha
tusubiri tuone jinsi hali inavyokuwa. Kama Rigathi Gachagua ndiye alikuwa
shida, ndio mlikuwa mnaweka ushuru ukuwe juu si mpunguze sasa vile ametoka?”
Gachagua alisema.
Gachagua alibanduliwa ofisini mwezi uliopita baada ya
kushtumiwa kwa jumla ya mashtaka 11 ambayo yaliwasilishwa bungeni na mbunge wa
Kibwezi Magharibi, Mwengi Mutuse.
Baada ya kubanduliwa na seneti, aliyekuwa waziri wa
masuala ya ndani, Kithure Kindiki aliapishwa wiki mbili baadae kama naibu rais
mpya katika ukumbi wa KICC.
Kindiki aliapa kutomuangusha rais Ruto katika
kuendesha serikali yake, akiahidi kufanya kazi sako kwa bako, bega kwa began a bosi
wake katika kutimiza manifesto yake ya 2022.
Kuapishwa kwake kulikuwa kumechelewa baada ya
mawakili wa Gachagua kuelekea mahakamani kupinga kubanduliwa kwake na bunge la
seneti.
Comments 0
Sign in to join the conversation
Sign In Create AccountNo comments yet. Be the first to share your thoughts!